Jumapili, 15 Juni 2014

MAKAM MKUU WA CHUO SEKOMU ATOA MOTISHA KWA WANACHUO

Ni ijumaa ya tarehe 13/06/20014 alipokutana na wanachuo wote wa mwaka wa kwanza hadi wa tatu. Akiwa anaongea na wanafunzi wa chuo wa mwaka wa kwanza aliwataka kutokukubali makundi yanayoweza kuvunja umoja wetu. Pia alisisitiza nidhamu upendo na ushirikiano.

Makam mkuu wa chuo Dr.Aneth Munga amewapa motisha wanachuo wa mwaka wa kwanza kuwa wajitahidi kwa bidii zote kujifunza lugha ya alama kwani pinid watakapokuwa na uhitaji wa mkalimani kwa ajili ya kuwassaidia wale wenye matatizo ya kusikia wapatikane kwa urahisi. Alisema "Najua watahitaji mshahara, sisi tutakachofanya sehemu ya ada yao tutawambia wasilipe na hiyo ndiyo itakayokuwa kama mshahara wao". Hivyo kauli hii sio kwa mwaka wa kwanza tu bali ni kwa wanachuo wote wasomao lugha ya alama na wasiosoma.















Hakuna maoni:

Chapisha Maoni